Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) –ABNA– Walimu na wanafunzi wa Ofisi ya Al-Mustafa Zanzibar wamekusanyika katika kikao maalumu cha khatmu ya Qur'an Tukufu kwa ajili ya kumuombea rehema na daraja za juu kiongozi shahidi wa Umma wa Kiislamu, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, pamoja na Mashahidi wote wa Vita vya Ramadhani.

Washiriki wa kikao hicho walisoma Qur'ani Tukufu, wakamwomba Mwenyezi Mungu Awajaalie mashahidi hao rehema, msamaha na daraja ya juu Peponi, huku wakisisitiza umuhimu wa kuendeleza mshikamano wa Kiislamu, kushikamana na mafundisho ya Qur'ani na kuenzi kujitolea kwa mashahidi katika kulinda dini na haki.

Kikao hicho kilihitimishwa kwa dua maalumu ya kuwaombea Waislamu amani, umoja na ushindi dhidi ya dhuluma.

Your Comment